“WWE” Kuandaa Pambano Kati ya nyota wa klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo dhidi ya John Cena

Estimated read time 1 min read

Kampuni inayojihusisha na michezo ya mieleka duniani maarufu kama “WWE” ina mpango wa kuandaa pambano kati ya nyota wa klabu ya Al Nassr Cristiano Ronaldo dhidi ya nguli wa mchezo huo wa mieleka John Cena kama sehemu ya uzinduzi wa mashindano ya mieleka yanayojulikana kama “Crown Jewel” ambayo yanatarajiwa kufanyika nchini Saudi Arabia Novemba 4 mwaka huu.

Unaambiwa baada ya kulipeleka soka Saudi Arabia, sasa ni zamu ya Ronaldo kuipeleka mieleka nchini humo.

Kwa mujibu wa Talk Sports, Cristiano Ronaldo huenda akacheza kwenye mchezo wa mieleka itakayoandaliwa na (WWE) kwa mara ya kwanza pamoja na Mwanamieleka na Mwigizaji maarufu Duniani, John Cena kwenye onyesho la “Crown Jewel” linalotarajiwa kufanyika Novemba 4, 2023 Nchini Saudia Arabia.

Share this post

You May Also Like

More From Author

+ There are no comments

Add yours