Klabu ya Yanga imefungiwa kusajili mpaka itakapomlipa mchezaji Gael Bigirimana raia wa Burundi. Uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai dhidi ya klabu hiyo.
Bigirimana alifungua kesi FIFA kuhusiana na malipo ya ada ya usajili (sign on fee). Yanga ilitakiwa iwe imemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini haikutekeleza hukumu hiyo. Wakati FIFA imeifungia Yanga kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeifungia kufanya uhamisho wa ndani.
TFF imezikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili.
Iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu.
Kupitia MwanaHabariNews
+ There are no comments
Add yours