Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje Chirau Ali Mwakwere sasa ndiye msemaji wa Jamii ya Digo.
Mwakwere alichaguliwa katika wadhifa huo na jamii yenye makao yake kaunti ya Kwale baada ya msako wa mwaka mzima wa kumtafuta mfalme.
Aliyekuwa Mbunge wa Msambweni Marere wa Mwachai ndiye atakuwa naibu wake. Profesa Hassan Mwakimako alichaguliwa kuwa katibu. Mwakimako aliwaambia waandishi wa habari kuwa uongozi huo mpya unaojulikana kwa jina la “Ngambi” unatarajiwa kuunganisha jumuiya hiyo ambayo ilikumbwa na mfarakano wa miaka mingi.
+ There are no comments
Add yours