Akiwa kahifadhi tuzo zake mbili kabatini. Ile ya Mtumbuizaji Bora wa Kike na Mwanamuziki Bora wa Kike. Ambazo alizitwaa wikiendi hii lakini hazijafanya ashindwe kuhoji.
Binti huyu mwenye asili ya Bububu na Paje katika visiwa vya Karafuu Zanzibar. Kahoji kama waandaaji wa tuzo yaani TMA, wanataka kumfurahisha kila msanii?
Ni katika ukurasa wake wa Insta, ndiko alikotundika maneno hayo. Bila shaka Zuchu alitamani kukuche haraka ili atoa nyongo yake. Ni kipi kilimsibu hata kudiriki kuandika hayo?
“Ni muhimu sana mijadala ya tuzo ikaanza kwa maendeleo ya Tasnia. Tanzania Music Award hongereni sana kwa kuendelea kuboresha, lakini inabidi kamati ijibu maswali kadhaa ya je, mnataka kubalance mzani na kutaka kufurahisha kila msanii au mnachotazama ni nini?”
Hayo ndio maneno ya @officialzuchu katika ukurasa wake wa Instagram.
+ There are no comments
Add yours