Hapo jana wafuasi wa bongo movie na mashabiki wa aliyekuwa movie star wa Filamu za kibongo marehemu Steven Kanumba, waliweza kuadhimisha mwongo mmoja tokea kufariki kwake
Steven Kanumba alizaliwa January 8, 1984, katika familia wa Wasukuma katika mkoa wa Shinyanga kaskazini mwa Tanzania. Alikuwa maarufu sana kwa kazi ya filamu na televisheni na kuitwa nyota maarudu zaid Tanzania (Steven Kanumba The Great)
Alifanya kazi nyingi ndani na nje ya nchi na amewahi fanya kazi na mwigizaji maarufu wa Nigeria Ramsey Nouah, filamu iliyotambulika kama ‘DEVILS KINGDOM’
Anatambulika kwa filamu nyingi za kiswahili kama Oprah, A Point of No Return, Lost Twins, Red Valentine, Love & Power, Neno La Mwisho, Big Daddy, Deception, The stolen will, Johari na zinginezo.
Alicheza filamu ya Love & Power na Ndoa Yangu mwaka wa 2012 kabla ya kifo chake
Kanumba ndiye mwigizaji wa kipekee nchini Tanzania aliyeshinda tuzo nyingi na taaluma yake ilichukua zaidi ya muongo mmoja. Baadi ya tuzo alizoshinda ni kama Muigizaji bora wa mwaka 2006, muigizaji bora Tanzania 2007, Tuzo ya msanii bora mwaka wa 2008
Aliwahi kuwa mgeni maalum kwa shindani la Big Brother Africa 4 mwaka wa 2009 na pia kuteuliwa kuwa balozi wa OXFAM GROW nchini Tanzania mwaka wa 2011. Kanumba alifariki tarehe 7 April, 2012 baada ya kusemakana alisukumwa na mpezi wake, Elizabeth Lulu, na kuanguka kufuatia ugomvi waliokuwa nao.
+ There are no comments
Add yours